Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Migogoro lazima itafutiwe ufumbuzi ukanda wa Sahel: Ban

Migogoro lazima itafutiwe ufumbuzi ukanda wa Sahel: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa BanKi-moon ambaye yuko ziarani katika ukanda wa Sahel, hii leo amehutubia katika bunge nchini Niger na kulitaka taifa hilo kuungana na nchi nyingine za ukanda huo kutafuta suluhu za migogoro huku akipendekeza kile alichokiita ni muarubaini wa migogoro.

Halikadhalika katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameliambia bunge la Niger kuwa hakuna amani bila maendeleo na maendeleo hayawezi kuwa endelevu kama hakuna amani huku pia akieleza nia ya umoja huo katika kuisaida nchi hiyo kuimarisha utawala bora na ujenzi wa taasisi muhimu za kitaifa.