Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwawezesha wanawake kutunza maliasili ni muhimu katika amani endelevu:Ripoti UN

Kuwawezesha wanawake kutunza maliasili ni muhimu katika amani endelevu:Ripoti UN

Ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa njia bora ya kuziwezesha nchi zilizokumbwa na mizozo ya kivita kurejea kwenye amani na kusonga mbele kimaendeleo ni kwanza kuwawezesha wanawake kupata fursa ya kumilika rasilimali ikiwemo ardhi, maji,misitu na madini.

Ripoti hiyo imebainisha nchi ambazo zimetumbukia kwenye mizozo ya kivita wanawake ndiyo wanaochukua jukumu la kwanza la kufanikisha upatikanaji wa hudumu muhimukamamaji, chakula na nishati ili kuiwezesha jamii kukithi matakwa yake.

Imeelezwa pia baadhi ya nchi ikiwemo huko Sierra Leone wanawake wanawajibika katika kazi ngumu kama zile za misituni na kazi za ufundi mchundo.

Pia inakadiriwa wanawake ndiyo wanaochukua zaidi ya asilimia 90 ya wale wote wanaojishughulisha na shughuli za uchimbaji mdogo wa dhahabu.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa pamoja na mchango mkubwa walionao wanawake lakini jambo la kushangaza  ni kwamba bado wameendelea kutengwa kwenye mabaraza ya utoaji maamuzi na suala la umiliki wa vyanzo vya rasilimali ikiwemo ardhi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la wanawake UN Women Phumzile Mlambo-Ngcuka alisema kuwa wanawake ndiyo waathirika wakubwa na vita.

Amesema kuwa jamii inapaswa kutambua umuhimu wa kumshikirikisha mwanamke kwenye mabaraza ya maamuzi na kumpa fursa ya kumiliki vyanzo vya rasilimali kwani kwa kufanya hivyo kutafanikisha ujenzi wa taifa.