Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Virusi vingine vipya vya AH7N9 vyazuka Uchina:WHO

Virusi vingine vipya vya AH7N9 vyazuka Uchina:WHO

Kamishna ya afya ya uzazi wa mpango nchini China imeliarifu shirika la afya ulimwenguni WHO juu ya kubainika kwa watu wawili wapya ambao wamegundulika kukumbwa na virusi vya AH7N9 kufuatia uchunguzi wa kimaabara uliofanywa dhidi yao. George Njogopa na taarifa kamili

 (TAARIFA YA GEOERGE NJOGOPA)

Mgonjwa wa kwanza kugundulika kukumbwa na virusi hivyo ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 3 ambaye alikuwa amekaribiana na banda la kuku.

Mtoto huyo kutoka jimbo la Guangdong kwa mara ya kwanza aliugua Oktoba 29 na baadaye akakimbizwa katika hospitali moja baada ya kupita siku mbili.Kwa sasa hali ya afya yake imeelezwa kuwa ni njema.

Mgonjwa wa pili alikuwa mama mwenye umri wa miaka 64 kutoka jimbo la Zhejiang. Naye pia alikuwa na tabia ya kukaribiana na mifugo yake aina ya kuku. Alianza kuugua Oktoba 30 na siku iliyofuatwa alikimbizwa hospitalini. Hali yake imeelezwa kuwa bado ni mbaya.

Hadi sasa shirika la afya ulimwenguni limepokea ripoti za kimaabara 139 ambazo zimedhibitisha watu waliougua kutokana na virusi hivyo, ikiwemo vifo 45.

Kwa sasa wagonjwa sita wamelazwa na wengine 88 wameruhusiwa kutoka hospitalini.

Katika hatua zake za awali za kukabiliana na kuenea kwa virusi hivyo, serikali ya China imeweka chini ya uangalizi mkali baadhi ya maeneo