Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawakwamua watoto waliosafirishwa Uganda

IOM yawakwamua watoto waliosafirishwa Uganda

Shirika la Kimataifa la uhamiaji nchini Uganda IOM, limefanikiwa kuwarejesha katika sehemu zao za asili watoto 21 ambao walikumbwa na biashara haramu  ya usafirishaji wa binadamu.

Kwa mujibu wa IOM zoezihiloambalo linaendeshwa kwa ushirikiano na serikali yaUgandahususani vyombo vya dola pia linahusisha mafunzo maalum kwa watoto hao kabla ya kuwarejesha nyumbani. Katika mahojiano na Joseoh Msami wa idhaa hii msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe anaanza kwa kueleza kinachofanywa na shirika hilo katika kutekeleza suala hilo.

(SAUTI JUMBE-MAHOJIANO)