FAO yahaidi kuwapiga jeki wakulima waliokumbwa na mafuriko Benin

5 Novemba 2013

Shirika la chakula na kilimo FAO limewapiga jeki wakulima waliopoteza mazao yao kaskazini mwa Benin wakati mto kingo cha mto Niger zilipopasuka na kusababisha uharibifu mkubwa wa mashamba na mifugo.

Hali hiyo iliyojitokeza mwezi Agust mwaka huu ilikuwa kama vile kutonesha kidonda kwa wakulima hao ambao walikuwa wakianza kupata afuheni kutokana na mafuriko yaliyowakumba msimu uliopita.

Akiwa katika siku yake ya kwanza ya ziara yake nchini Benin, Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva alisema kuwa shirika hilo liko tayari kunyosha mkono wa usaidizi kwa waathirika hao. Katika mazungumzo yake na mwenyeji wake rais Yayi Boni, Graziano da Silva alipongeza hatua zilizopigwa na Benin hasa katika eneo la ufikiaji wa malengo ya maendeleo ya mellenia.

Kwenye ziara yake hiyo José Graziano da Silva anatazamiwa pia kuzindua mpango maalumu wenye lengo la kusisaidia familia zilikumbwa na mafuriko kuinuka upya

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter