Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uharamia pembe ya Afrika wakusanya karibu dola Milioni 400: Ripoti

Uharamia pembe ya Afrika wakusanya karibu dola Milioni 400: Ripoti

Utafiti mpya kuhusiana na mwenendo wa vitendo vya uharamia umebaini kuwa takriban dola Milioni 400 zilikusanywa kutokana na vitendo hivyo katika kipindi cha kati ya Aprili 2005 na Disemba 2012. Pia utafiti huo umebainisha kuwa kiasi cha meli 179 zilitekwa katika Pwani ya Somalia na eneo la Pembe ya Afrika katika kipindi hicho hicho. George Njogopa na ripoti kamili.

(Taarifa ya George)

Utafiti huo ulioendeshwa kwa pamoja kati ya shirika la uhalifu la kimataifa, Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa madawa ya kulevya na uhalifu na Benki ya Dunia ulikuwa na shabaha ya kubaini mtitiririko wa fedha chafu zinazopitishwa kwa njia ya panya baada ya kufanyika kwa vitendo vya kihalifu katika eneo la Pembe ya Afrika. Utafiti huo ulikusanya takwimu katika nchi zaDjibouti,Ethiopia,Kenya, Usheli Sheli naSomalia. Pamoja na kubainisha ukubwa wa tatizohilo, utafiti huo umesema kuwa wakati dunia ikiwa katika karne ya 21,kundi la maharamia waSomaliasiyo tu kwamba limeendelea kuzusha kitisho kwenye eneohilo, lakini pia hujuma zao zimesambaa na kuvuruga ustawi wa dunia. Stuart Yikona ndiye aliyeandika ripoti ya utafiti huo

 (Sauti ya Stuart)

Aidha amependekeza hatua za kuchukuliwa.

(Sauti ya Stuart)