Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maonyesho ya nchi za Kusini yakamilika Nairobi

Maonyesho ya nchi za Kusini yakamilika Nairobi

Maonyesho ya wiki moja ya miradi na mbinu za maendeleo zinazojali mazingira yaliokuwa yakifanyika mjini Nairobi, Kenya yakihusisha nchi zinazoendelea yamefungwa hii leo . Maonyesho hayo yaliandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia ushirikiano wa nchi zinazoendelea, SOUTH-SOUTH. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Maonyesho hayo yaliwaleta pamoja zaidi ya wajumbe 800 kutoka pembe mbali mbali za dunia na zaidi ya makundi 50 yaliyokuwa yakionyesha uvumbuzi wao na  yakizihusisha nchi zinazoendelea ambapo uchumi wa nchi hizo unachangia asilimia 47 kwenye biashara ya dunia.

Akizungmza wakati wa kukakimila kwake rais wa baraza kuu  la Umoja wa Mataifa John W Ashe amesema kuwa maonyesho hayo yamekuwa ya manufaa makubwa katika kuhakikisha kuwa malengo ya milenia ya mwaka 2015 yameafikiwa

(Sauti ya Ashe)

Samson Gichia ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Cobitech Biogas mjini Nairobi ni mmoja wa wale waliotuzwa wakati wa maonyesho hayo baada ya kubuni mbinu ya kuunda gesi ya kupikia kutoka kwa taka ikiwa ni mbadala wa matumizi ya kuni.

(Sauti ya Samson)