Hali bado ni tete Jamhuri ya Afrika ya Kati

1 Novemba 2013

Kiasi cha raia milioni 1.1 katika Jamhuri ya Kati ikiwemo asilimia 50 ya raia waliokosa makazi kutokana na machafuko yanayoendelea wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula. Wengi waliokimbia makazi yaowanadaiwa kujificha msituni kwa hofu ya kushambuliwa.

Mahitaji ya misaada ya kibinadamu yameongezeka katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni kutokana na kuzuka upya kwa machafuko hayo ambayo yamezorotesha maeneo mengi. Kuanzia mwezi Marchi mwaka huu kumeshuhudiwa hali ngumu ikiongezeka kwa mamia ya familia na baadhi ya mipango ya utoaji mahitaji ya kujikimu imevurugika.

Inakadiriwa kwamba kiasi cha watu 395,000 bado wameendelea kukosa makazi kutokana na  machafuko hayo. Shirika la chakula duniani WFP linasema kuwa ili kufanikisha mipango yake ya usambazaji wa chakula, kiasi cha dola za Marekani milioni 20 zitahitajika.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud