Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaendesha tathimini kuwasaidia wakimbizi wa DRC

IOM yaendesha tathimini kuwasaidia wakimbizi wa DRC

Wakati kukiwa na taarifa ya waasi wa kundi la M23 wanaopambana na jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kwa usaidizi wa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kuweka utulivu nchini humo MONUSCO kujisalimisha, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linafanya tathimini ya namna ya kuwasaidia wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo , DRC, waliokimbia mapigano ya hivi karibuni mashariki mwa nchi hiyo ambapo idadi kubwa inasemekana wamekimbilia nchi jirani ya Uganda. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM

(Sauti Jumbe)