Udhibiti bora wa maji ni muhimu kwa kujenga uhimili katika eneo la Sahel

31 Oktoba 2013

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

Udhibiti bora wa maji ndiyo njia bora ya kujenga uhimili wa watu katika eneo la Sahel barani Afrika, na ya kuzinusuru jamii za vijijini kutokana na matatizo ya chakula yanayotokana na ukame ambayo yamelikumba eneo hilo katika miaka ya hivi karibuni.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula, FAO, José Graziano da Silva, wakati wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu uhimili wa eneo la Sahel, ambao umeangazia unyunyiziaji mashamba maji na udhibiti wa maji. Mkutano huo umewajumuisha washirika kutoka nchi za Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania, Niger, na Senegal.

Bwana da Silva ametoa wito wa uwekezaji zaidi katika kilimo, ili kufungua milango ya utajiri uliopo.

Mafuriko na ukame ni changamoto ya mara kwa mara kwa maisha ya wakulima na wafugaji katika eneo la Sahel, na hivyo kufanya maji kuwa tatizo kubwa, yawe kwa wingi au haba, katika eneo ambalo limetajwa kuwa mojawapo ya maeneo yaliyo hatarini zaidi. Bwana da Silva amesema watu fukara zaidi ndio walio hatarini zaidi, na ndio wanaoathiriwa zaidi.

Watu wa eneo la Sahel hutegemea sana kilimo kiuchumi, na hivyo kutegemea sana mashamba, maji na nyasi za malisho, lakini hali ya rasilmali hizo imekuwa ikizoroteka kutokana na kupanua makazi ya wanadamu, mmomonyoko wa udongo, na mahitaji ya chakula, malisho ya mifugo, kuni na maji.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter