Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakala wa Nuklia Japan watoa ufafanuzi wa IAEA

Wakala wa Nuklia Japan watoa ufafanuzi wa IAEA

Wakala wa udhibiti matumizi ya nyuklia nchini Japan umetoa ripoti kuelezea hali ilivyo katika kinu cha Fukushima ambacho hivi karibuni kiliripotiwa kujitokeza kwa hitalafu iliyozusha wasiwasi wa kuibuka mionzi mikali.

Katika ripoti yake kwa wakala wa Umoja wa Mataifa wa silaha za nyuklia IAEA, Japan imesema kuwa imefanikiwa kufuatilia kwa karibu hali ilivyo kwenye vinu vya Fukushima ambavyo miaka kadhaa iliyopita vilizusha sokomoko kubwa kufuatia mafuruko na tetemeko lililotingisha Japan.

Wakala hiyo imesema kuwa pamoja na mvua kubwa zilizonyesha hali bado ni ya kuridhisha kwani uchunguzi uliofanywa kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye kina kirefu cha bahari umebaini kutojitokeza kwa kasoro zozote.

Hapo majuzi wakala hiyo ilitoa taarifa iliyoelezea matengenezo yaliyofanywa kwenye vinu hivyo ikiwemo kuchukua tahadhari kutokana na uwezekano wa kujitokeza kwa kimbunga Typhoon Francisco.