Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa Afrika kuendelea kukua mwaka 2014

Uchumi wa Afrika kuendelea kukua mwaka 2014

Nchi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara zinatazamiwa kuendelea kupata mafanikio ya kiuchumi katika msimu wa mwaka ujao 2014 tofauti na hali iliyoshuhudiwa katika kipindi cha mwaka 2013, limesema Shirika la fuko la fedha duniani IMF.

IMF imeeleza kuwa mafanikio hayo ya kiuchumi ni matokeo ya kuwepo kwa mazingira bora barani Afrika na nje ya bara hilo.

Geroge Njogopa na taarifa kamili.

(Taarifa ya George)

Katika ripoti yake iliyoelezea hali ya uchumi kwa nchi za Kusin mwa Jangwa la Sahara, IMF imesema kuwa kuongezeka kwa kasi ya uwekezaji katika eneo hilo kumetoa msukumo mkubwa wa ukuaji wa hali ya uchumi katika mataifa mengi.

Ripoti hiyo inasema hali ya uzalishaji inatazamiwa kupanda kwa wastani wa asilimia 5 kwa mwaka huu 2013 na inaweza kuongezeka pia katika mwaka ujao wa 2014 hadi kufikia asilimia 6.

Akitangaza ripoti hiyo, Mkurugenzi wa IM kwa kanda ya Afrika Bi Antoinette Sayeh,amesema kuwa pamoja na kujitokeza kwa mikwamo ya hapa na pale, lakini hali jumla ya uchumi inatazamiwa kuendelea kuimarika.

Hata hivyo nchi hizo za Afrika zimeonywa kutobweteka na matokeo hayo mazuri kwani zinaweza kujikuta zikitumbukia kwenye mazingira magumu iwapo kutajitokeza mabadiliko ya hali ya hewa ama hitilafu za kisiasa.