WFP, UNHCR yatangaza kupunguza chakula kwa wakimbizi Kenya

31 Oktoba 2013

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la wakimbizi UNHCR na lile la mpango wa chakula WFP yametangaza kwamba kuanzia Novemba mosi yatalazimika kupunguza kiwango cha mgao wa chakula kwa wakimbizi zaidi ya nusu milioni katika kambi za Daadab na Kakuma nchini Kenya kutokana na upungufu wa rasilimali.

Taarifa ya pamoja ya mashirika hayo imesema hatua hii imefanyika baada ya hatu zote za kunusru hali ya chakula kukwama na hivyo kuamua kupunguza asilimia 20 ya chakula kwa mwezi Novemba na Desemba kwa lengo la kuhakikisha ziada ya chakula ghalani inatosha hadi mwisho wa mwaka na kutaka wafadhili kusaidia katika kunusuru mamia kwa maelfu ya wakimbizi watakaoathirika na punguzo hilo la chakula.