Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu atiwa wasiwasi na hali nchini Bangladesh

Katibu Mkuu atiwa wasiwasi na hali nchini Bangladesh

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa akifuatilia hali ilivyo huko Bangladesh na amesema ana wasiwasi mkubwa juu ya ongezeko la ghasia ambazo zimesababisha vifo vya watu kadhaa na wengi wamebaki majeruhi.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wake imemkariri akitaka pande zote kujizuia na kuheshimu utawala wa sheria huku wakitoa maoni yao kwa amani. Bwana Ban amesema ni matumaini yake kuwa hatua za hivi karibuni za kuitisha mashauriano zitaendelea na amezitaka pande zote kuhakikisha kuna mazingira yanayowezesha kufanyika uchaguzi halali na kwa amani.