Brahimi bado yuko Damascus, Kaag kuhutubia Baraza la Usalama wiki ijayo

30 Oktoba 2013

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu kuhusu Syria Lakhdar Brahimi yuko nchini humo ambapo leo amekuwa na mazungumzo na Rais Bashar Al Assad. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amesema tayari Brahimi amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid al-Moallem na anaendelea na vikao na wawakilishi wa vikundi mbali mbali vya upinzani, vikundi vya wanawake na vile vya kiraia.

Nesirky amesema Ijumaa hii Brahimi atazungumza na waandishi wa habari mjini Damascus na hatimaye ataelekea Beirut kwa mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo akiwemo Rais, Waziri Mkuu na spika wa bunge.

Wakati huo huo Nesirky akaelezea ratiba ya kazi ya mratibu maalum wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na shirika la kimataifa la kupinga matumizi ya silaha za kemikali, OPCW Sigrid Kaag.

(Sauti ya Martin)

“Bi. Kaag amenieleza kuwa atakutana na Mkurugenzi mkuu wa OPCW na watendaji wengine waandamizi huko The Hague, kesho na baadaye ataelekea Moscow kwa mkutano na viongozi wa Urusi Ijumaa, Bi. Kaag atakuwepo New York kupatia taarifa baraza la usalama wiki ijayo.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter