Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Fatiha Serour msaidizi mwakilishi wake nchini Somalia

Ban amteua Fatiha Serour msaidizi mwakilishi wake nchini Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon ametangaza uteuzi wa Fatiha Serour raia wa Algeria kuwa msaidizi wa mwakilishi wake maalum kwa ajili ya Somalia

Bwana Ban amemshukuru Peter De Clercq wa Uholanzi ambaye emitumikia nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Somalia, UNSOM. Mteule huyo mpya Bi . Serour ana uzoefu katika maswala ya diplomasia ya kimataifa kwani amefanya kazi na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usadizi nchini Afgahnstan UNAMA na kwa sasa ni mkurugenzi wa taasisi inayojihusisha na masuala ya usawa na ujumuishaji .

Bi Serour ana shahada ya uzamivu katika maswala ya mikakati ya maendeleo barani Afrika na shahada ya uzamili katika maswala ya mahusiano ya kimataifa.