Nchi za Afrika hazitoi ushirikiano wa kutathmini hali ya haki za binadamu: Kiai

30 Oktoba 2013

Mtaalam maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kufanya mikutano ya amani na haki ya kujumuika, Maina Kiai, ametoa wito kwa nchi za Afrika zishirikiane naye na wenzie katika kufanya tathmini ya hali ya haki za binadamu katika nchi hizo.

Katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Kiai, amesema katika muktadha wa uchaguzi, haki za watu hukiukwa kote duniani, lakini ulimwengu huangazia tu siku ya uchaguzi yenyewe, na mara nyingi kutangaza kuwa uchaguzi umekuwa huru na wa haki, bila kuangalia ikiwa vyama vya upinzani vinaruhusiwa kufanya mikutano au mashirika ya umma kushiriki ipasavyo.

Akiangazia nchi za bara la Afrika, amesema wataalamu wa haki za binadamu wanapata changamoto kubwa, kwani mara nyingi nchi hizo hazitoi mwaliko wowote kwao kwenda kukagua hali ya haki za binadamu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter