Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini Tanzania mimba za utotoni hali yasalia tete: UNFPA

Nchini Tanzania mimba za utotoni hali yasalia tete: UNFPA

Ripoti hiyo ambayo imeangazia hali ya idadi ya watu imesema kuwa kati ya mimba milioni moja zinazotungwa nchini Tanzania, basi asilimia 23 za mimba hizo zinawahusu wasichana walio chini ya umri wa miaka 19. Taarifa zaidi na George Njogopa:

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 Kulingana na ripoti hiyo, idadi ya watoto wa kike wanaopata mimba bado ni kumbwa na kwamba takwimu za sasa zinaonyesha kuwa kila kwenye wasichana 10, basi 4 kati yao wamepata mimba.

 

Baadhi ya mambo yaliyotajwa kusababisha hali hiyo ni pamoja na kuwepo kwa mila potofu ambazo zinawakandamiza na kuwabagua watoto wa kike.

 

Jambo jingine lililoelezwa na ripoti hiyo ni kuendelea kuongezeka kwa ndoa za utotoni ambazo hutumika kama kigezo cha kujipatia mali kwa baadhi ya wazazi.

Akielezea zaidi kuhusiana na hali hiyo, Afisa wa UNFPA anayeshughulika na afya ya uzazi Dorothy Temu Usiri kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, tayari kumeanzisha kampeni zinazotaka kuangaliwa kwa sheria ya ndoa ambayo itaruhusu mtoto wa miaka 15 kuolewa.