Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama kuu nchini Maldives inavuruga shughuli ya uchaguzi : Pillay

Mahakama kuu nchini Maldives inavuruga shughuli ya uchaguzi : Pillay

Kamishina Mkuu wa haki zaa binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea wasi wasi wake kutokana na mabadiliko ambayo yametokea kwenye shughuli ya uchaguzi chini Maldive kufuatia hatua ya mahaka kuu nchini humo ya kuingilia uchaguzi wa urais.

Taarifa kamili na Jason Nyakundi

(TAARIFA YA JASON)

Pillay amesema kuwa kuna wasi wasi mkubwa kuwa mahakama kuu nchini Maldives inaingilia uchaguzi wa urais hatua ambayo imetajwa kuwa inakandamiza demokrasia na kukiuka haki ya wananchi wa Maldive ya kuwachagua kwa njia ya haki waakilishi wao. Mahakama kuu ilitupilia mbali awamu ya kwanza ya uchaguzi wa urais tarehe 7 mwezi Septemba mwaka huu kufuatia madai kuwa ulikumbwa na utata, hata baada ya waangalizi wa kimataifa kutangaza kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki. Pillay amesema kuwa mahakama iliiwekea tume ya uchaguzi mipangilio ambayo itakuwa vigumu kuitimiza hali ambayo ilisabaisha polisi kuizuia tume hiyo kundaa awamu ya pili ya uchaguzi ambao ungefanyika taehe 19 mwezi huu. Pillay pia amesema wanachama wa tume ya haki za binadamu nchini Maldive wamekuwa wakitishiwa maisha ukiwemo uvamizi wa mwezi huu dhidi ya kutuo cha runinga kinachomilikiwa na upinzani.