UNHCR yaonya kufuatia hatua ya kuwarejesha kwa lazima wale wanaokimbia ghasia nchini Nigeria.

29 Oktoba 2013

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa raia wa Nigeria wanaokimbia ghasia kaskazini mashariki mwa nchi hawatarejeshwa makwao kwa lazima. Alice Kariuki na ripoti kamili.

 (Ripoti ya Alice)

Mapigano kati ya wanajeshi wa Nigeria na wanamgambo kwenye majimbo yaliyo kaskazini mashariki mwa nchi ya Adamawa, Borno na Yobe yamewalazimu hadi watu 10,000 kuhama makwao wengi wakiwa wamevuka mpaka na kiuingia nchi majirani za Cameroon,Chad na Niger. UNHCR inazitaka nchi majirani kufungua mipaka yao kwa raia wa Nigeria wanaokimbia ghasia hizo ikiongeza kuwa wengi wao huenda wanahitaji usalama wa kimataifa na misaada ya kibinadamu. Dan McNorton ni msemaji wa UNHCR mjini Geneva.

"Ghasia zinakadiriwa kusababisha kuhama kwa watu 5000 katika eneo hilo, huku huduma za kibindamu zikiwa zimetatizwa UNHCR inaamini kuwa idadi ya watu walioathiriwa huenda ikawa ni ya juu. UNHCR imetiwa  wasi wasi na ripoti za watu 111 waliolazimika kurudi Nigeria kutoka Cameroon tarehe 5 mwezi huu. Watu hao walifukuzwa kutoka kijiji kilicho kaskaazini mwa Cameroon kwenda jimbo la Adamawa nchini Nigeria. Wakati wa kisa hicho watu 15 waliuawa na wengina saba wakajeruhiwa. Waliosalia 89 walirejea tena Cameroon na kuzuiliwa. UNHCR inashirikiana na serikali ya Cameroon kubaini iwapo kuna watu wanaohitaji usalama wa kimataifa."

Majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria ya Adamawa, Borno na Yobe yamekuwa chini ya hali ya hatari tangu mwezi Mei mwaka huu wakati serikali inapoendelea kupambana na wanamgambo wa  kundi la Boko