UNESCO yaanzisha kampeni ya kuzuia maambukizi ya HIV miongoni mwa vijana

29 Oktoba 2013

Shirika la  Umoja wa Mataifa linalohusika na Sayansi, Elimu na Utamaduni UNESCO limesema kuwa zaidi ya ailimia  50 ya vijana ambao tayari wamefikia umri wa kubalehe walioko katika nchi za Kusini na Afrika Mashariki hupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kila siku kutokana na kukosa elimu bora ya uzazi.

Kutokana na hatua hiyo, UNESCO imeanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya kutoa msukumo kwa nchi kuhakikisha kwamba mitaala ya elimu inakidhi viwango vya elimu ya uzazi itakayowasaidia vijana hao kufanya maamuzi pindi watapojihusisha na masula ya mapenzi. George Njogopa na taarifa zaidi.

(Taarifa ya George)

Ikiwasilisha utafiti wake iloufanya katika nchi 21 zilizoko Kusini na Mashariki mwa Afrika, UNESCO imebaini juu ya kukosekana kwa mitaala maalumu juu ya afya ya uzazi jambo ambalo linawafanya vijana wengi kukosa maamuzi sahihi pindi wanapojitumbukiza kwenye hatua za kimapenezi.

Akizungumzia matokeo ya utafiti huo, Mtaalamu wa UNESCO Mathias Faustini alisema kuwa pamoja na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa ili kukabiliana na tatizo la mimba shuleni na upunguzwaji maambukizi ya virusi vya HIV kwa vijana, lakini uzoeefu umeonyesha kuwa juhudi hizo zimekosa mikakati ya kisanyansi.

Utafiti huo umefadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa UNAIDS, UNICEF, WHO, UNFPA

Kutokana na hali hiyo baadhi ya wanafunzi wametoa ushauri wa mamlaka za dola wakitaka kupatiwa mitaala inayokwenda na wakati