Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya chakula nchini Zimbabwe yasalia kuwa mbaya: WFP

Hali ya chakula nchini Zimbabwe yasalia kuwa mbaya: WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linasema hali ya uhakika wa chakula nchini Zimbabwe ni mbaya zaidi tangu uhaba wa chakula kukumba nchi hiyo mwaka 2009. WFP inasema uhaba wa chakula unatokana na sababu kadhaa ikiwemo hali mbaya ya hewa, gharama kubwa ya mbolea na hata upatikanaji wake ni wa taabu pamoja na kupanda kwa bei ya vyakula kunakochochewa na matarajio ya mavuno madogo.

Tayari serikali ya Zimbabwe imeomba msaada wa kimataifa wa chakula ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka kila uchao. Inaelezwa kuwa kati ya mwezi Januari na Machi 2014 idadi ya watu wanaohitaji msaada wa chakula itaongezeka na kufikia Milioni Mbili nukta mbili.   Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

 (Sauti ya Byrs)