Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani shambulio la M23 dhidi ya MONUSCO

Baraza la usalama lalaani shambulio la M23 dhidi ya MONUSCO

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu limekuwa na kikao cha dharura na faragha kuhusu hali ilivyo Mashariki mwa DR Congo ambako mapigano mapya yamezuka Ijumaa alfajiri kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23 na kusababisha vifo.

Taarifa iliyotolewa baada ya kikao hicho imekariri wajumbe wakilaani vikali mashambulio yaliyofanywa na M23 dhidi ya MONUSCO hadi kusababisha kifo cha afisa kutokaTanzaniaambapo wametuma rambirambi kwa familia ya mlinda amani huyo na serikali ya Tanzaniapamoja na MONUSCO.

Halikadhalika wametuma rambirambi kufuatia vifo vya raia huko DR Congo pamoja na hukoRwandaambako makombora yameripotiwa kutua.

Wajumbe wametaka serikali ya DR Congo kuchunguza haraka tukiohilona wahusika wafikishwe mbele ya sheria huku wakisema wanaunga mkono MONUSCO na kutaka pande zote husika kupatia ujumbe huo ushirikiano wa kutosha.

Mapema Mwakilishi wa kudumu wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Balozi Gerard Araud alielezea kile kilichotokea hadi afisa wa Tanzania kuuawa wakati kikosi cha MONUSCO kilipokuwa kikisaidia jeshi la DRCongokulinda raia huko Kiwanja-Rutshruru, kilometa 25 kaskazini mwa Goma kwa mujibu wa mamlaka iliyopatiwa.

 (Sauti ya Balozi Araud)

 “Wakati wanafanya hivyo, afisa mmoja wa Tanzania alipigwa risasi na mpiganaji wa M23. Ni kwamba alikuwa amevaa kofia ya kujihami lakini risasi ilimpiga kwenye koo. Na kuhusu kombora kutua Rwanda, Baraza la usalama lililaani Ijumaa."