Lang Lang balozi mpya wa amani wa UM

28 Oktoba 2013

Mwanamuziki chipukizi kutoka China Lang Lang ameidhinishwa rasmi kuwa balozi wa amani wa Umoja wa Mataifa tukio lililofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwamo Katibu Mkuu Ban Ki-moon ambaye licha ya kumsifia mwanamuziki huyu anaainisha majukumu yake akiwa balozi wa amani.

 

"Lang Lang atafanya kazi nasi katika moja ya vipaumbele vyangu vikuu , elimu kimataifa. Juhudi zangu za elimu kimatifa zinajielekeza katika malengo matatu, la kwanza, kuwaingiza shuleni watoto kote duniani, bado tuna watoto milioni 57 wnaostahili kwenda shule duniani ambao hawajajiunga shuleni inabidi tuwawezeshe, pili ni kuboresha kiwango cha kujifunza na kukuza uraia wa kimataifa."

Akizungumza katika mahojiano maalum balozi huyo mpya wa amani wa Umoja wa Mataifa Lang Lang anasema

"Ni heshima kuwa balozi wa amani mdogo kuliko wote. Nhitaji kujifunza kutoka kwa mabalozi wengine na kuongea na Bwana Ban ili niwe balozi mzuri wa amani. Nitajitahidi kufanya kazi kwa bidii kuichukua nafasi hii na nina matumaini tutaleta tofauti."