Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi zaidi kutoka DRC wamiminika nchini Uganda

Wakimbizi zaidi kutoka DRC wamiminika nchini Uganda

Zaidi ya watu 3,000 kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamekimbilia nchi jirani ya Uganda baada ya vijiji vyao kushambuliwa na waasi wanaodaiwa kuwa ni wa M18.

John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, ana ripoti kamili.

(Tarifa ya John Kibego)

 Wakimbizi hao ambao wamekuwa wakiingia kutoka wilaya ya Aru mkoani Orintale kwanzia tarehe 19 mwezi huu, sasa wako katika wilaya ya Koboko inaayopakanisha Uganda na Sudan Kusini kwa upande wa kaskazini na DRC kwa upande wa magharibi.

Wakimbizi hao wamesema walilazimika kutoroka makwao baada ya vijiji vyao kushambuliwa na wasi wa M18 wanaodaiwa kuongozwa na Lt. Col. Zachariah Ndozi ajulikanaye sasa kama Eric.

Shalom Ayukuru Mkuu wa ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) ya Arua, amesema tayari wameanza kuwasaidiya wakimbizi hao kwa kuwapa chakula na maji miongoni mwa mahitaji mengine.

 (sauti ya Shalom Ayukuru)

Wengi wao walikimbia muishoni mwa wiki, wakipitia barabara tofauti na wengine vichakani.

Wakimbizi wa DRC wamekuwa wakimiminika humo nchini katika miezi ya hivi karibuni kufuatia kuongezeka mapigano kati ya jeshi la serikali na makundi tofauti yaliyojihami.

Kundi la M23 limewalazimisha maelfu kutoroka majumbani katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, FARDC likiwakimbiza maelfu kotoroka wilaya ya Ituri na wengine ni hao wanaotoroka M18 lililojitokeza mwezi Machi mwaka huu.