Tutafungua ofisi Misri kusaidia mchakato wa katiba: Pillay

25 Oktoba 2013

Umoja wa Mataifa unatarajia kufungua ofisi ya kanda nchini Misri kwa ajili ya kusaidia nchi hiyo katika machakato wa kuandika katiba. Katika mahojiano maalum na Dob Bob wa idhaa ya Kingereza ya radio ya Umoja wa Mataifa mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navy Pillay amesema bado hali ya usalama ni tete nchini Misri na amekuwa akipokea taarifa za vifo na majeruhi na kusisitiza uwepo wa Umoja wa Mataifa nchini humo utasadia keleta suluhisho kwa nchi hiyo iliyoko Kaskazini mwa Afrika

 "Naendelea kupokea ripoti ya vifo na kujeruhiwa kwa waandamanaji  lakini natarajia kupokea kwa ukunjufu mwaliko wa serikali wa kufungua ofisi ya kikanda yenye mamalaka ya kusimamia ili tuweze kuisadia serikali katika mchakato wake wa kuandika katiba. "