Hali ya Abyei yatia wasiwasi: Baraza la Usalama:

24 Oktoba 2013

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mashauriano ya faragha kuhusu Sudan na Sudan Kusini ambapo wajumbe wameeleza wasiwasi wao juu ya ongezeko la mvutano huko Abyei.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mashauriano hayo, Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi Oktoba Balozi Agshin Mehdiyev kutoka Azerbajian amesema wajumbe wametaka kila pande kujizuia ili kuepusha mvutano zaidi na hata kukwamisha jitihada za kuleta suluhu.

Amesema wajumbe pamoja na kupongeza mazungumzo ya hivi karibuni kati ya Marais wa nchi mbili hizo, wametaka jamii husika kutumia vyema ziara ya ujumbe wa Umoja wa Afrika huko Abyei ili kuweza kumaliza tofauti kati yao.

(Sauti ya Balozi Mehdiyev)

Halikadhalika amesema wanasubiri taarifa kutoka baraza la amani na usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kile walichokiona na kusongesha mbele harakati za pande husika kumaliza mgogoro huko Abyei.