Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni lazima tukuze viwanda na biashara kuinua uchumi wa Afrika :AU

Ni lazima tukuze viwanda na biashara kuinua uchumi wa Afrika :AU

Wakati wiki ya Afrika ndani ya Umoja wa Mataifa ikiendelea mjini New York mwangalizi wa kudumu wa Ujumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa Tete Antonio amesema ili kufikia malengo ya kiuchumi ni lazima bara hilo libadilishe mfumo na kukuza viwanda na biashara.

Katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Bwana Antonio ambaye hata hivyo amesema anaridhishwa na hatua za ukuaji wa uchumi barani Afrika

(Sauti Antonio)

Ukuaji wa bara hili ulisalia kwenye aslimia tano licha ya mdororo wa kiuchumi duniani na kuna mabadiliko mengi ya muundo hata katika mitizamo, tunahitaji kujikita katika viwanda, tumekuiwa tukisafririsha mlighafi kwa karne kadhaa lakini haijaleta tija kama ajira kuna haja ya kubadilisha namna ya kufanya biashara ili kuwatosheleza idaidi kubwa ya watu ambao ni vijana na ni mtaji