Tanzania yaadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa

24 Oktoba 2013

Nchini Tanzania, kilele cha wiki ya Afrika na Umoja wa Mataifa kimeshuhudia hii leo jijini DSM kama anavyoripoti mwandishi wetu George Njogopa.

(Ripoti ya George)

 Akizungumza wakati wa kilele cha madhimisho hayo, Mwakilishi Mkazi  wa Umoja wa Mataifa nchini Alberic Kacou alisema kuwa ni fahari ya Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku hii wakati dunia ikipiga hatua kuelekea kufikia maelengo ya maendeleo ya melenia ambayo ukomo wake ni mwaka 2015.

Alisema kuwa pamoja na kwamba kumekuwa na changamoto kubwa kuyafikia malengo hayo lakini baadhi ya nchi zimeanza kupiga hatua kubwa ikiwemoTanzaniaambayo inapongezwa kwa kufanya vyema katika baadhi ya maeneo.

Kwa upande mwingine alitoa shukrani na pongezi kwa serikali ya Tanzania namna inavyoendelea kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa kuleta amani sehemu zenye mizozo.

 "Ningependa kuchukua nafasi hii kuishukuru Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuunga mkono vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Mataifa. Lakini pia ningependa kuchukua fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru na kutoa maombi yetu kwa mashujaa wa kitaifa waliopoteza maisha."

Kwa hivi sasa Tanzania inashiriki operesheni ya pamoja inayoratibiwa na Umoja wa Mataifa huko Mashariki kwa Jamhuri ya Kongo kwa ajili ya kuwafurusha wanamgambo wa M23.

Akizungumza kwenye sherehe hizo, Waziri wa maliasili na utalii Khamis Kagasheki aliye mwakilishi Waziri wa Mambo ya Nje, alisema kuwa kauli mbinu ya mwaka huu inayotoa msukumo wa ustawi wa vijana imekuja wakati muafaka kwani inajadiliwa katika wakati ambapo mataifa mengi yanaanza kuweka kipaumbele kwa ustawi wa vijana hao.

 Lakini pia aligusia kuhusiana na wiki ya Umoja wa Mataifa ambayo kileleche kimefikia leo.

"Sherehe za wiki ya Umoja wa Mataifa ni jambo muhimu kwani inasaidia kuwaelimisha watu wetu kuhusu Umoja wa Mataifa na shughuli zake nchini Tanzania na duniani kote."

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter