Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yasafirisha misaada ya madawa na chakula kwa watoto nchini Syria

UNICEF yasafirisha misaada ya madawa na chakula kwa watoto nchini Syria

Ndege iliyokodishwa  na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF inayobeba madawa yanayohitajika kwa dharura nchini Syria na chakula cha wototo  imewasili mjin iBeirut ambapo misaada hiyo itasafirishwa kwa njia ya barabara kwenda Syria. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(Taarifa ya Jason)

Ndege hiyo ilibeba karibu tani 28.6 za misaada  ya chakula ma madawa ya chanjo kwa watoto walio kati ya umri wa miezi 6 na 23. Mwakilishi nwa UNICEF nchini Syria Youssouf Abdel-Jelil anasema kuwa kampeni hiyon ni muhimu kwa kuwa inawafikia watoto ambao walikuwa wamekosa chanjo siku za nyuma. Abdel – Jelil anasema kuwa usafirishaji wa misaada kwa njia ya ndege ndiyo njia ya  haraka zaidi akiongeza kuwa chakula hicho kitawasaidia watoto wanaotaabika nchiniSyria.

Mwakilishi huyo wa UNICEF amesema kuwa changamoto zinazotokana na watu kuhama na kupanda kwa bei ya chakula pamoja na uhaba wa chakula maeneo mengine, ni masusla ambayo yamekuwa na athari kwa lishe ya watoto huku msimu wa baridi unaokuja ukitarajiwa kuichochea zaidi hali hiyo. UNICEF inasema kuwa itakuwa ikiwalenga watoto 50,000 kwa kipindi cha miezi mitatu inayokuja kwenye sehemu zilizo athirika zaidi nchini Syria.