Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahofia ghasia kati ya serikali na Renamo huko Msumbiji

Ban ahofia ghasia kati ya serikali na Renamo huko Msumbiji

Kuongezeka kwa ghasia kati ya vikosi vya serikali na wafuasi wa chama cha RENAMO nchini Msumbiji kunazidi kumtia hofu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye katika taarifa amenukuliwa akitaka pande zote kujizuia kufanya vitendo vyovyote vinavyoweza kutishia amani. Amerejea makubaliano ya Roma ya mwaka 1992 ambayo amesema yameleta amani iliyodumu kwa miaka 21 sasa na hivyo ni lazima yakazingatiwa.  Katibu Mkuu amesihi serikali na RENAMO kumaliza tofauti zao kupitia mbinu shirikishi na za kidemokrasia zilizowekwa ili kuhakikisha Msumbiji inaendelea kufikia maendeleo endelevu yanayojumuisha watu wote.