Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani shambulio nchini Mali

Baraza la usalama lalaani shambulio nchini Mali

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio ililofanywa na kundi lenye silaha lisilofahamika dhidi ya  askari walinda amani chini Mali katika kizuizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha amani nchini Mali MINUSMA, na kusababisha vifo vya askari kadhaa raia wa Chad na raia wengine kufa na kujeruhiwa. Katika taarifa yake  kwa waaandishi wa habari mjiniNew Yorkbaraza hilolimetuma salamu  za rambirambi kwa familia za askri waliopoteza maisha, serikali yaMali,Chadna MINUSMA. Baraza la usalama limesisitiza kutoa ushirikiano kwa MINUSMA na vikosi vya jeshi la Ufaransa vinavyounga mkono MINUSMA. Kadhalika baraza limesisitiza kwamba watekelezaji wa shambuliohilowatawajibishwa na kuitaka serikali yaMalikuanzisha uchunguzi hima na kuwafikisha wahusika katika vyombo vya sheria.