Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumejizatiti kutokomeza kemikali chafuzi: Tanzania

Tumejizatiti kutokomeza kemikali chafuzi: Tanzania

Kamati ya mkataba wa kimataifa wa Stockholm unaofuatilia kemikali chafuzi imependekeza kupigwa marufuku kwa matengenezo, matumizi na usambazaji wa aina mbili za kemikali zitumikazo katika kuhifadhi mbao, kwenye rangi na kuua wadudu.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo kemikali hizo ni PCN na HCBD ambapo kutaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na nchi zinazoendelea kujihami dhidi ya madhara ya kemikali hizo, Joseph Msami wa idhaa hii amefanya mahojiano kwa njia ya simu na Mkurugenzi wa Mazingira katika ofisi ya Makamu wa Raisi nchini Tanzania Dk Julius Ningu anayeanza kwa kuelezea mafunzo maalum kwa wataalamu wa viwandani, kilimo na mifugo yanayolenga kujihami na kemikali hizo.