Ripoti za APRM zinatia matumaini changamoto ni utekelezaji: Balozi Ndangiza

23 Oktoba 2013

Wiki ya Afrika ndani ya Umoja wa Mataifa inaendelea kwenye mjini New York, ambapo Makamu Mwenyekiti wa jopo la watu mashuhuri linalosimamia mpango wa Afrika wa kujitathmini wenyewe, Balozi Fatuma Ndangiza amesema ripoti za tathmini ni nzuri lakini kitendawili ni utekelezaji.

Akizungumza katika mahojiano maalum na kituo hiki kando mwa mkutano na waandishi wa habari, Balozi Ndangiza amesema ripoti hizo pamoja na kutaja changamoto za nchi husika kama vile rushwa, demokrasia, hubainisha pia mpango wa kitaifa wa kutekeleza ili kushughulikia changamoto hizo. Hivyo akapendekeza kile cha kufanya….

(Sauti ya Balozi Ndangiza)

Balozi Ndangiza akazungumzia kile kinachoonekana ukuaji wa uchumi kutofikia wananchi wote….

(Sauti ya Balozi Ndangiza)

Miaka 10 baada ya kuanzishwa kwa APRM, nchi 33 zimeridhia mpango huo na tayari 17 zimefanyiwa tathmini ikiwemo Kenya, Rwanda, Tanzania na Ghana.