Idadi ya wagonjwa wa Kifua Kikuu Tanzania ni kubwa kuliko makadirio: Dkt. Kamara

23 Oktoba 2013

Ripoti mpya ya WHO kuhusu ugonjwa Kifua Kikuu iliyotolewa Jumatano imeonya uwezekano wa kutoweka mafanikio yaliyopatikana kwenye tiba dhidi ya ugonjwa huo. Hofu hiyo inatokana na uwezekano wa wagonjwa Milioni Tatu duniani kote kuwa nje ya mifumo ya tiba na janga la Kifua Kikuu sugu kuendelea. NchiniTanzaniamafanikio  yaliyopatikana ni pamoja na kupungua kwa maambukizi mapya miongoni mwa vijana lakini kuna changamoto. Je ni zipi hizo? Assumpta Massoi wa Idhaa hii alizungumza kwa njia simu na Kaimu Mkuu wa mpango wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini Tanzania Dokta Deus Kamara ambaye kwanza anaanza kwa kueleza jipya waliloliona kwenye utafiti wa hivi karibuni ambapo takwimu za makadirio ya wagonjwa ni za chini kuliko hali halisi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter