Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulizi dhidi ya askari walinda amani Mali

Ban alaani shambulizi dhidi ya askari walinda amani Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio lililofanywa na watu wasiojulikana dhidi ya askari walinda amani chini Mali katika kizuizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha amani nchini Mali MINUSMA, na kusababisha vifo vya askari kadhaa raia wa Chad na raia wengine kujeruhiwa.

 Katika taarifa yake  kwa waaandishi wa habari mjini New York Bwna Ban ametoa salamu zake za rambirambi kwa familia za askari waliopoteza maisha na kuwatakia uponyaji wa haraka raia waliojeruhiwa.

Bwana Ban amesema shambuliohilo halitarudisha nyuma nia ya Umoja wa Mataifa kusaidia kuimarisha usalama, utulivu na amani endelevu nchini Mali.