Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya mafanikio kuna changamoto katika TB; Tanzania tafiti zaibua mapya:

Licha ya mafanikio kuna changamoto katika TB; Tanzania tafiti zaibua mapya:

Ripoti iliyochapishwa leo na shirika la afya ulimwenguni WHO imeonyesha mafanikio ya tiba dhidi ya kifua kikuu ikiwemo kuokoa maisha ya watu zaidi ya Milioni 22 duniani kote huku idadi ya wagonjwa ikipungua hadi kufikia watu milioni 8. Mwaka jana. Hata hivyo ripoti hiyo inaonya uwezekano wa kutoweka kwa mafanikio hayo. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(TAARIFA YA GRACE)

Takwimu hizo mpya zinaleta matumaini kuhusiana na hatua za ufikiaji wa malengo ya maendeleo ya milenia hasa lile la kupunguza ugonjwa wa kifua kikuu ambao unaziandama zaidi nchi zinazoendelea kutokana na mazingira ya wakazi wake. Hata hivyo WHO inataja mambo yanayoweza kupeperusha mafanikio hayo kuwa ni Mosi ni wagonjwa Milioni Tatu dunini kote kutofikiwa na mfumo wa afya wa kitaifa na hivyo penginepo kushindwa kupata tiba na pili ni janga la kifua kikuu sugu, MDR-TB ambapo WHO inasema kuwa uwezo wa kuwapima na kuwatibu wenye kifua kikuu sugu hautoshelezi. Dkt Karin Weyer ni kutoka WHO.

(Sauti ya Dkt. Weyer)

“Hatuna madaktari wa kutosha wa kukabiliana na ugonjwa sugu wa kifua kikuu. Ni ngumu. Wagonjwa wanapata athari ambazo zinapaswa  kuangaliwa. Na tunaona kwamba kuna upungufu wa wahudumu wa afya. Hii inasababisha  vifo vya wengi na wanosubiri matibabu wanaendelea kueneza ugonjwa sugu wa kifua kikuu.”

Nchini Tanzania utafiti uliofanyika hivi karibuni  umebaini idadi kubwa zaidi ya wagonjwa kuliko makadirio ya awali. Dkt. Deus Kamara ni Kaimu Mkuu wa mpango wa Kifua Kikuu na Ukoma.

 (Sauti ya Dokta Kamara)