Biashara haramu ya mbao Bonde la mto Congo yapatiwa muarobaini

23 Oktoba 2013

Nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa mbao, pamoja na wawakilishi wa sekta hiyo wameridhia makubaliano ya kupambana na biashara haramu ya mbao kwenye bonde la mtoCongo. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO kufuatia mkutano wa kimataifa uliofanyika mjini Brazaville. Taarifa ya Jason Nyakundi inafafanua zaidi.

 

 (Taarifa ya Jason)

Likiwa na ukubwa wa ekari milioni 300 bonde la mtoCongo ndiko kuliko msitu wa pili kwa ukubwa duniani na pia eneohilo linaongoza kwa kuwa na biashara haramu ya mbao inayogharimu serikali karibu dola bilioni 10 kila mwaka. Wakati wa mkutano huo washirika walridhia nyaraka ambapo waliahidi kushirikinana kuhakisha kuwa sekta ya mbao imehalalishwa katika eneohilo . Mathalani kutekeleza hatua za kufuatilia mbao na kuwepo uwazi na usimamizi wa misitu. FAO inasema makubaliano hayo ya Brazaville yatasaidia kapunguza uharibifu wa misitu wakati huu ambapo makadirio yanaonyesha kuwa msitu waCongo hupoteza ekari 700,000 za miti kila mwaka kuanzia mwaka 2000 hadi 2010.