Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii asilia zataka kushirikishwa katika mipango ya maendeleo

Jamii asilia zataka kushirikishwa katika mipango ya maendeleo

Wakati mikutano mbalimbali ya jamii za watu asilia ikichukua kasi mjini New York, kilio kikubwa cha jamii hiyo ni namna miradi ya rasilimali asilia inavyoathiri watu hao hususani barani Afrika pamoja na mitizamo hasi ya serikali kwa kundihilo.

 Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa, mwenyekiti wa jukwaa la kimataifa la watu wa asili Paul Kanyinke Sena amesema ni muhimu jamii hizo zihusishwe katika kupanga mipango ya maendeleo itakayohusisha ardhi wanakoishi ili kupunguza migogoro inayoweza kuepukikwa.

 Hata hivyo Bwana Sena amesema mitizamo hasi ya serikali kwa jamii ya watu ailia inachochea kutoelewana miongoni mwa pande hizo na kusisitiza ushirikishwaji wa kundihilo.

 (Sauti - mahojiano na Sena)