UM wavitaka vyama kinzani kusitisha mashambulizi Msumbiji

22 Oktoba 2013

Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa makini hali ya kuzorota kwa usalama nchini Msumbiji na umetoa wito kwa pande zinazokinzana kusitisha mapigano hima na kuanzisha majadiliano ya kumaliza tofauti ili kujenga demokrasia ya kweli na maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amesema Umoja huo una taarifa za kuzorota kwa amani kufuatia taarifa za shambulio lililofanywa na wapiganaji wa chama cha upinzani nchini Msumbiji dhidi ya serikali ya chama tawala Frelimo na kusisitiza

(Sauti ya Martin Nesirky)

"Tunafuatilia kwa makini hali ya hivi karibuni nchini Msumbiji na tunatoa wito kwa vyama vyote kujiepusha na vitendo vinavyotishia amani ambayo imetawala nchini humo kwa miaka 21 iliyopita, tunavitaka vijumuike katika majadiliano ya kuondoa tofauti zao na kuhakikisha nahi inaendelea katika njia ya maendeleo,demokrasia na ukuaji jumuishi.Ni kweli Katibu Mkuu alidhuru Msumbiji hivi karibuni na hivyo anafuatailia kwa makini maendeleo ya nchi hiyo."