Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO, Bangladesh zazindua mpango wa kulinda sekta za viwanda vya nguo

ILO, Bangladesh zazindua mpango wa kulinda sekta za viwanda vya nguo

Serikali ya Bangladesh kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la ajira, ILO, limezindua mpango wa juhudi za kuboresha usalama sehemu za kazi kwa wafanyakazi wa sekta za viwanda vya nguo nchini humo.

Mpango huo unaogharimu dola za kimarekani milioni 242 unalenga katika kupunguza hatari za moto na kuanguka kwa majengo katika viwanda na kuhakikisha haki na usalama wa wafanyakazi. Mpango huo unaungwa mkono kadhalika na Uingereza na Uholanzi ambapo nchi hizo zimechangia dola milioni 15 .

Hii ni sehemu ya kuchukua tahadhari kufuatia idadi kadhaa ya ajali zilizokabili sekta ya viwanda vya nguo nchini Bangladesh