Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria inatoa ushirikiano kwenye uteketezaji wa silaha zake za kemikali: Bi.Kaag

Syria inatoa ushirikiano kwenye uteketezaji wa silaha zake za kemikali: Bi.Kaag

Mratibu maalum wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na OPCW ya kusimamia uteketezaji wa mpango wa silaha za kemikali nchini Syria, Sigrid Kaag yuko nchini humo kufuatia uteuzi wake hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa hii leo imemkariri akisema kuwa changamoto ni kumaliza kazi ndani ya muda uliopangwa ambao ni katikati ya mwaka ujao. Bi. Kaag amesema hadi sasa serikali ya Syria imetoa ushirikiano wa kina kusaidia kazi ya ujumbe huo na ametoa shukrani kwa serikali hiyo na hata wananchi wa Syria.

Halikadhalika amesema kitendo cha Syria kujiunga na mkataba wa kupinga matumizi ya silaha za kemikali ni ishara kuwa imeazimia kutekeleza kazi ya kutokomeza silaha hizo.