Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wakwamisha usambazaji misaada Syria, huku msimu wa baridi kali ukikaribia

Mzozo wakwamisha usambazaji misaada Syria, huku msimu wa baridi kali ukikaribia

Mzozo unaoendelea nchini Syria unazidi kutatiza jitihada za huduma za kibinadamu wakati msimu wa baridi unapowadia. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa kwa mwaka  hu pekee karibu asilimia 35 ya misaada yake imeendea watu walio kwenye maeneo yaliyo vigumu kufikiwa kamaAleppo, Azzaz na Karameh. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.

 

 (Taarifa ya Alice)

UNHCR inasema kuwa kwa kila wiki karibu malori 250 yaliyo na misaada huwa safarini ndani mwaSyriayakiwapelekea misaada kati ya familia14,000 na 15000 au karibu watu 100,000 kila wiki.

Hata baada ya kufanywa kwa jitihada kama hizi mahitaji ndani mwaSyriani makubwa huku watu zaidi wakiendela kuhama makwao.

Kwa sasa Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kuna zaidi ya watu milioni 4.25 waliolazimika kuhama ndani mwaSyria  na huenda idadi hiyo ikaongezeka. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

(Sauti ya Adrian)

 

 

Mapema mwezi huu tulianza kusambaza bidha za msimu wa baridi kote nchini Syria yakiwemo mablanketi ya joto na turupa za platiki za kuwasaidia mamilioni ya watu waliahama makwao. Tumerekebisha mahema yanayowahifadhi watu 35,000 kati ya watu 80,000 tunaoelenga kuwafikia kabla ya msimu wa baridi.