Jamii asilia zalalama kuathiriwa na miradi ya rasilimali

21 Oktoba 2013

Mikutano mbalimbali kuhusu haki za jamii za watu asilia inaendelea mjini New York huku suala la umiliki wa raslimali likigubika mijadala  hiyo  ambapo mwenyekiti wa  jukwaa la kimataifa la watu wa asili Paul Kanyinke  Sena amesema watu wa asili huathirika pakubwa hususani barani Afrika pale serikali inapotaka kundeleza miradi ya raslimali asilia  mathalani mafuta na gesi.

 Katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Bwana Sena amesema ni lazima jamii asilia zihusihwe katika  majadiliano kabla ya utekelezaji wa miradi hiyo.

 (Sauti Sena)

 Akizungumzia nafasi ya jamii za watu asilia katika mpango wa mikakati ya maendeleo baada ya 2015 Bwana  Sena amesema

 (Sauti Sena)

 Katika kupaza sauti ya jamii ya watu asilia, wanawake wa jamii hizo kutoka nchi zaidi ya mia mbili kote duniani watakutana mwishoni mwa mwezi wa tano nchini Peru kujadili namna wanavyokosa huduma muhimu za kijamii ikiwamo afya, na namna wanavyoathirika na migogoro mbalimbali.