Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utata wa mpaka baina ya Guyana na Venezuela kupata suluhu

Utata wa mpaka baina ya Guyana na Venezuela kupata suluhu

Tarehe 17 mwezi huu mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya utata wa mpaka baina ya Guyana na Venezuela Bwana Norman Girvan  amekuwa na mikutano tofauti na mawaziri wa mamabo ya nje wa Guyana na Venezuela.

Mawaziri hao wamesisitiza kwamba kuna mahusiano mazuri ambayo yanaendelea baina ya mataifa hayo mawili. Wakikumbushia hatua zilizopigwa na ofisi zao siku za nyuma mawaziri hao wamekaribisha mapendekezo ya mwakilishi huyo maalumu ya kuchukua hatua zaidi kushughulikia utata wa suala la mpaka.

Hatua hizo zitajumuisha mlolongo wa mikutano kusukuma mbele mchakato katika miezi ijayo. Mwakilishi huyo amesema ametiwa moyo na nia ya pande zote mbili kujitahidi kupata suluhu chini ya mwamvuli wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.