Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala kufanyika Tanzania kuona iwapo fursa zilizopo zatumika vyema: UM

Mjadala kufanyika Tanzania kuona iwapo fursa zilizopo zatumika vyema: UM

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa, YUNATZ, wameandaa mjadala wa wazi kuhusu dunia itakiwayo baada ya mwaka 2015 wakati malengo ya maendeleo ya milenia yatakapofikia ukomo. Usia Nkhoma-Ledama Afisa kutoka kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo amezungumzia mjadala huo wa Jumanne tarehe 22 ambao ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchiniTanzania.

(Sauti ya Usiah)