Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti za awali zaonyesha kuwepo kwa polio Syria

Ripoti za awali zaonyesha kuwepo kwa polio Syria

Shirika la afya ulimwenguni WHO limepokea ripoti juu ya kujitokeza kwa matukio yanayohusiana na ugonjwa wa polia nchini Syria.

Waataalamu wa afya wamesema kuwa wamebaini kuwepo kwa ashirio la ugonjwa huo lilibainika mwezi huu wa Oktoba katika jimbo la Deir Al Zour na kwamba uchunguzi zaidi umeanza kuchukuliwa.

Taarifa zilizopatikana kutoka maabara ya Mjini Damascus zimeashiria uwezekano wa kuwepo kwa ugonjwa huo wa polia baada ya uchunguzi wa awali kubaini .Mara ya mwisho ugonjwa wa polia uliropotiwa nchini Syria mwaka 1999.

WHO limewataka wale wote wanaotoka nchini humo ama kwenda huko kuzingatia kupata kinga dhidi ya ugonjwa huo.