Ban apokea matokeo ya awali Guinea, ataka amani.

18 Oktoba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepokea matokeo ya awali ya uchaguzi wa kisheria nchini uliofanyika tarehe 28 September nchini Guinea, yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo CENI.

Katika taarifa yake Bwana Ban ameongeza serikali ya Guinea, taasisi zake na washikadau wote kwa mchango wao kwa taasisi na kwa kufanya uchaguzi. Pia ameshukuru juhudi endelevu za chuo cha uwezeshaji na kamati ya ufuatiliaji wa makubaliano ya July 31 kuhusu uratibu wa uchaguzi, chini ya uongozi wa mwakilishi wake maalum Afrika Magharibi.

Pia Bwana Ban amesema ana matumaini amani itaendelea kutawala na kuvitaka vyama vyote kudumisha utulivu na kutatua migogoro yote kwa njia za kisheria. Katibu huyo Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameihakikishia Guinea kwamba UM utaendelea kuisadia nchi hiyo katika juhudi za kuimarisha utawala wa kidemokrasia na taasisi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter