Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM, EU zapinga biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu

IOM, EU zapinga biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linaungana na nchi za Jumuiya ya Ulaya na washirika wake kwenye ukanda huo kwenye maadhimisho ya saba ya kupinga biashara haramu ya usafirishaji binadamu.

Biashara hiyo haramu ya pili kwa ukubwa baada ya ile ya mihadarati ni miongoni mwa changamoto kubwa za ukiukwaji wa haki za binadamu na huhusisha takribani watu laki nane  kwa mwaka wanaovushwa katika mipaka ya nchi. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM na anafafanua kinachofanywa katika maadhimisho hayo.

 (Sauti Jumbe)