Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yataka kukomeshwa kwa madini ya risasi za kuta kuwalinda watoto

WHO yataka kukomeshwa kwa madini ya risasi za kuta kuwalinda watoto

Shirika la afya ulimwenguni WHO limeanzisha juhudi za kukomeshwa kwa uzalishaji na matumizi ya rangi za kung’arisha ikiwemo kuta na wanasesere ambazo zina madini ya risasi kwa kuwa imebainika kuwa na athari kubwa kwa afya za watoto hasa kwenye ubongo wao. George Njogopa na ripoti kamili

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

WHO inasema kuwa zaidi ya asilimia 99 walioathiriwa na sumu hiyo wanakutikana katika nchi zenye kipato cha chini na kile cha kati na ikikadiriwa kuwa karibu watoto 600,000 hupata matatizo ya ubungo kila mwaka kutokana na sumu hiyo.

Ving’arisho vya aina ya risasi vinatajwa kuwa na athari kubwa kwa maisha ya watoto ambayo hupatikana maeneo ya nyumbani, kwenye midoli na sehemu nyingine.

Katika kuelekea kwenye kilele cha wiki ya kupinga matumizi yake, inayofanyika kila mwaka kuanzia Oktoba 20 hadi 26,WHO imezitolea mwito nchi kuchukua hatua madhubuti kutokomeza matumizi yake.

Mkuruguenzi wa afya ja jamii wa WHO DrMaria Neira, amesema kuwa kuendelea kuiachia sumu hiyo ni hatari kwa afya za watu

(SAUTI YA DR MARIA NEIRA)

"Athari za madini ya risasi ni zipi kwa binadamu? Madini ya risasi itakuwa na madhara makubwa kwa ubongo na mfumo wa mishipa ya fahamu kisha inaweza kusababisha kukosa fahamu, degedege na hata kifo. Jambo baya kabisa ni kuwa watoto ambao wameathriwa na madini ya risasi watakuwa na uharibifu wa akili na matatizo ya tabia maisha yao yote. Hakuna tiba."